Ruto afutilia mbali kuwepo kwa kundi la ‘Deep State’ lenye ushawishi kwenye uchaguzi mkuu 2022

Naibu Rais William Ruto amefutilia mbali uwepo wa kundi almaarufu deep state lenye ushawishi kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe tisa Agosti mwaka huu. Ruto ambaye leo amekita kambi katika eneo la magharibi haswa kaunti ya Kakamega na Bungoma sasa ametoa changamoto kwa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kujiandaa kikamilifu kukabailiana naye debeni akimshtumu kuwa mpango wa kisiasa wa mabwenyenye. Ruto amewaonya wakaazi dhidi ya kushurutishwa kuunga mkono yeyote siasani.

関連記事

コメント

この記事へのコメントはありません。

TOP